Baada ya kufanya vizuri ndani ya mwaka jana, msanii wa bongofleva H-Baba,
amesema kuwa anatarajia kufungua mwaka huu na ngoma mpya inachowahusu
wanaume wanaopenda kutembea na wanawake bila malengo aliyoipa jina la ‘Funga Zipu’, ambayo hivi karibuni itakuwa hewani ambapo itakuwa sambamba na video.
Alisema kuwa kwa sasa anafanya utaratibu wa kutengeneza DVD
ambazo zitakuwa zinaonesha show zake zote alizopiga mwaka jana pamoja na
zile alizopiga na JB Mpiana msanii mahiri kutoka Congo, ambayo itakuwa sokoni mapema Februari mwaka huu.
H-Baba aliongeza
kuwa kutokana na tabia chafu walizonazo wasanii za kuibiana kazi sasa
anafanya utaratibu mpya kwa yeyote atakahusika na wizi wa kazi
zake atamchukulia hatua kali ikiwemo kumpeleka mahakani ili iwe fundisho
kwa wengine ambao wanashindwa kutumia akili zao badala yake wanasubiri
kuiba kazi ya mtu.
“Natarajia kufungua mwaka na kazi nyingi lakini ngoma yangu ya ‘Funga Zipu’ ndiyo itakayoanza
hivyo nawaomba mashabiki wangu ambao nipo nao miaka yote kuisubiri
kazi hiyo kwani ni hatari na hawa wanaopenda kuiba kazi zangu
watasubiri,” alisema.
H-BABA APANIA KUWAFUNDA WANAUME WANAOPENDA KUTEMBEA NA WANAWAKE BILA MALENGO NDANI YA NGOMA YAKE MPYA.

