MFANYABIASHARA, Mkumbukwa John Shayo (37) (pichani) aliyefariki katika
kifo chenye utata nchini China amezikwa Jumatano iliyopita na kulifanya
Jiji la Mwanza kutawaliwa na majonzi.
Umati wa watu ulihudhuria
mazishi hayo nyumbani kwa bibi wa marehemu, Mabatini kisha kuelekea
katika Makaburi ya Buzuruga, Nyakato na kila mtu alionekana kujawa na
huzuni.
Hata hivyo, mazishi hayo yaliathiriwa kidogo na mvua
iliyofanya baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki washindwe kuuaga mwili wa
marehemu.
Mkumbukwa alifariki China na maiti yake kuhifadhiwa
hospitali kwa takriban mwaka mzima na serikali ya nchi hiyo huku mkewe,
Neema Majukano pamoja na rafiki wa marehemu aitwaye Haji Msongore
wakilaumiwa kwa kushindwa kutoa taarifa mapema juu ya kifo hicho.
Aidha,
utata umegubika kifo cha Mkumbukwa kufuatia rafiki huyo wa marehemu
ambaye mara ya mwisho walikwenda wote nchini Chini kudaiwa kumuoa mke wa
marehemu, Neema.
MFANYABIASHARA ALIYEUAWA CHINA NA MAITI YAKE KUKAA MONCHWARI MWAKA MZIMA AZIKWA JIJINI MWANZA...

