Msanii wa filamu Bongo ambaye ni mke wa mtu, Chuchu Hans amefunguka
kuwa anatongozwa sana na wanaume kupitia Mtandao wa Kijamii wa
Facebook, kitendo kinachomkosesha amani.
Akizungumza hivi karibuni, Chuchu alisema kuwa, anachojua yeye mtandao
huo ni sehemu ya kukutana na marafiki na kubadilisha mawazo lakini cha
ajabu kila akiingia, wanaume kibao wamekuwa wakimtaka.
“Mimi kwa
kweli kila nikiingia Facebook nakutana na wanaume ambao wananitongoza,
mtu anajua kabisa una mtu wako lakini bila haya anatangaza dau na
kueleza kuwa, anakutaka, mijitu hii naichukia kweli,” alisema Chuchu.
NATONGOZWA SANA FACEBOOK-CHUCHU ATOBOA MAMBO!

