MASTAA
wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya na Blandina Chagula ‘Johari’
wametimkia nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ kwenda kurekodi filamu.
Irene Uwoya.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni kwa njia ya simu akiwa
nchini humo, Uwoya alisema wamekwenda nchini humo kurekodi sinema ambayo
Watanzania wataitambua ikikamilika. Pia wataunganisha na ziara ndefu
katika nchi mbalimbali barani Afrika zikiwemo Namibia, Ghana, Lesotho na
kwingineko kujifunza soko la filamu.
Blandina Chagula ‘Johari’.
“Tupo huku na Johari lakini tutakuwa na ziara ndefu sana ya nchi
mbalimbali za Afrika kwa ajili ya kulisogeza soko letu la filamu na
kujifunza jinsi wenzetu wanavyofanya katika filamu zao,” alisema Uwoya.