Muigizaji wa filamu nchini, Hemedy Suleiman aka PHD hivi karibuni
ataingia location kushoot filamu mpya iliyopewa jina la 90 Minutes
(Dakika 90).Katika filamu hiyo ya comedy, Hemed ataigiza na Mpoki.
“Nimepewa movie inaitwa 90mnts..soccer comedy movie!!…mimi captain
team ya mabishoo…mpoki captain team ya wagumu…daaah!!najiona RONALDO,”
alitweet PHD.
Akijibu swali kuhusu wasanii gani wengine wataokuwa kwenye
filamu hiyo na lini wataanza kushoot, Hemedy alijibu, “ndio casting
inatengenezwa…so far hiyo ndio info najua from the producer..More info
will alert you..location February.”
MPOKI NA HEMEDY NDANI YA FILAMU YA COMEDY IITWAYO----- 90 MINUTES

