Msanii nguli wa filamu za
Kibongo, Charles Magali ‘mzee Magali’ amesema kuwa anachukizwa na tabia
ya baadhi ya wasanii wa kiume wa filamu wanaojichubua na kuweka dawa
nywele zao.
Akizungumza na na mwandishi wa habari hii, mzee Magali alisema kwa muda mrefu amekuwa akilikemea jambo hilo bila ya mafanikio.
“Wasanii
ni kioo cha jamii, hebu waseme wanapata faida gani wanapofanya hivyo
zaidi ya kuhisiwa tofauti na jamii? Mbona wanaweza kuwa wasanii wazuri
bila ya kujichubua na kuweka dawa nywele zao?” alihoji.
"NAWACHUKIA SANA WASANII WA KIUME WANAOJICHUBUA"...MZEE MAGALI

