RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KUMZIKA JUMA KILOWOKO 'SAJUKI' JIJINI DAR LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki' leo.

Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam leo wamejitokeza katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam kumpumzisha mpendwa wao, Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki', aliyefariki dunia alfajiri ya Januari 2, mwaka huu (Jumatano) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Miongoni mwa waliomzika Sajuki ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mwili wa marehemu Sajuki ukishushwa kutoka kwenye gari.

Baba mzazi wa Sajuki, Mzee Kilowoko, akiweka udongo katika kaburi la mwanaye.



Mazishi ya Sajuki yakiendelea.


Twitter Delicious Facebook Digg Favorites More