STAA wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameeleza chanzo cha
wasanii Bongo kuigiza mapenzi kwenye filamu ni kwa sababu Tanzania
hakuna uhuru wa kuigiza.
Akizungumza hivi karibuni jijini Dar, Ray
alisema msanii anapoonesha kipaji chake kwa kuigiza kitu kwa ajili ya
kuelimisha jamii anarudishwa nyuma kwani wakati mwingine inafikia hatua
ya filamu husika kufungiwa.
“Hapa Tanzania hakuna uhuru wa kuigiza
kama zilivyo nchi nyingine ndiyo maana kila siku tunaigiza mapenzi tu.
Niliwahi kutoa filamu ya Second Wife (Mke wa Pili), Waislam
hawakunielewa mpaka baadaye. Juzikati nilitaka kutoa filamu ya Sista
Maria, Wakatoliki wameipinga isitoke, sasa nini kimebaki, ni kuigiza
filamu za mapenzi tu,” aliema Ray
RAY AELEZA SABABU ZA KUIGIZA MUVI ZA MAPENZI

