skip to main |
skip to sidebar

7:51 PM

Anonymous
Mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba,
Dk. Sengondo Mvungi leo asubuhi amepelekwa nchini Afrika Kusini kwa
matibabu zaidi. Dk. Mvungi alijeruhiwa vibaya na watu wanaosadikiwa kuwa
ni majambazi usiku wa Novemba 2 mwaka huu nyumbani kwake, Kibamba
jijini Dar es Salaam na alikuwa akipatiwa matibabu katika chumba cha
wagonjwa mahututi (ICU) katika kitengo cha MOI.