Mchekeshaji mkongwe, Amri Athuman ‘King Majuto’ hivi karibuni ataanza kuonekana kwenye kazi mpya iitwayo “Patashika”
Katika kazi hiyo iliyojaa vichekesho vya kuvunja mbavu, Majuto
atacheza kama baba wa familia mwenye vibweka vingi vya kustaajabisha,
vinavyowaacha watu hoi kila siku mtaani kwao.
“Nategemea kufanya kitu cha tofauti ili mashabiki waweze kujua mimi
ninaweza kuigiza ndiyo maana ninaigiza kama baba wa vibweka kwahiyo
wadau wangu wategemee vimbwenga vya kustajabisha” alisema gwiji huyo
wakuchekesha.
Mbali ya Majuto katika picha hiyo pia inawashirikisha nyota wengine
ambao ni wakonnge kwenye Nyanja za uchekeshaji wakiwemo Pembe, Senga,
Kingwendu, Full Tank na Difenda.
Kazi hiyo imepangwa kuingia sokoni hivi karibuni, ambako itapatikana mikoa yote hapa nchini, kwenye VCD pamoja na DVD
MZEE MAJUTO AJIPANGA KUTOKA NA "PATASHIKA" AMBAYO NI ZAIDI YA KOMEDI

