Kutokana na ndoa hiyo kuwa ya aina yake, hivi
karibuni waandishi wetu walimuweka kati Bob Junior na kumbana kwa maswali
ya “why, kwanini, ikawaje” aoe kimyakimya wakati yeye ndiye ‘prezidaa’ wa
masharobaro?
Bob Junior
akafunguka: “Nilifunga ndoa Desemba mwaka jana. Nililazimika kuoa kimyakimya
kutokana na masharti ya wazazi wa pande zote mbili kwamba ndoa isifungwe kwa
mbwembwe.”
Alisema, hata idadi ya wahudhuriaji katika ndoa hiyo ilidhibitiwa, hivyo kuruhusu ndugu na marafiki wachache kushuhudia tukio hilo.
Alisema, hata idadi ya wahudhuriaji katika ndoa hiyo ilidhibitiwa, hivyo kuruhusu ndugu na marafiki wachache kushuhudia tukio hilo.
“Kikubwa ni
kufunga ndoa inayompendeza Mungu ili atupe Baraka zake na tuishi katika maisha
yanayompendeza.
“Kwa Watanzania, napenda wajue tu ukweli kwamba nimeoa na mke wangu anatarajiwa
kujifungua hivi karibuni,” alisema Bob Junior a.k.a Mr. Chocolate.