Msanii wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ametoa
kali ya mwaka baada ya kueleza kuwa, mara nyingi hapendi kuhudhuria
kwenye misiba kwa kuogopa kulogwa.
Akiongea na mwandishi wa habari hii , msanii huyo alisema sehemu nyingi zenye
mikusanyiko ya watu ndiko wale walozi wanakofanyia kazi yao ya kuwaloga
watu ndiyo maana alikacha mazishi ya John Maganga, Mlopelo, Ramadhan
Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Juma Kilowoko ‘Sajuki’.
“Yaani mimi siku
hizi sipendi kabisa kwenda kwenye mikusanyiko ya wasanii na watu wengi
kwani huko ndiko tunamalizana hivihivi kwa kulogana. Japo vifo vya
wenzangu vimeniuma sana lakini sina la kufanya ila nawaombea kwa
Mungu,”alisema Baby Madaha.
"HUWA SIPENDI KUHUDHURIA MISIBA YA WATU MAANA NAOGOPA KUROGWA...!!!".BABY MADAHA

