MSHIRIKI wa Shindano la Maisha Plus Season II,
Jacqueline Dastan ‘Jack Maisha Plus’ na shosti wake ambaye ni bosi wa
Kundi la Nderemo Arts Group, Khadija Kasongo ‘Rubi’ wameanza kufanya
mazoezi ya viungo kwa lengo la kuondoa ‘vitambi’.
Wasanii hao
wameamua kuingia kwenye ‘tizi’ baada ya kuona vitambi vinakuwa tishio
kwao, jambo ambalo limekuwa likiwakosesha raha kwani wanahisi hawana
mwonekano mzuri.
Jacqueline Dastan ‘Jack Maisha Plus’.
“Tunafanya mazoezi asubuhi na jioni, lazima matumbo yapungue, si unaona
kama yameanza kupungua kidogo?” alisema Rubi ambaye siku za karibuni
aliwahi kuzichapa kavukavu na Jack kwa sababu ya kudaiana licha ya kuwa
ni marafiki wakubwa.
Pamoja na mazoezi hayo ya viungo, Rubi alisema
pia wanakunywa maji ya moto kila siku asubuhi ili kuyeyusha mafuta
mwilini na wanapunguza vyakula vyenye mafuta mengi.
“Usiku mara nyingi tunakula matunda tu badala ya chipsi kuku kama
zamani. Unajua mwanamke ukiwa na tumbo kubwa kwa kweli haupendezi
kabisa,” alisema Rubi.
Aliongeza kuwa ‘wachumba’ wengi siku hizi
hawapendi wanawake wenye ‘vitambi’ ndiyo maana wameamua kukomalia
mazoezi ili kujiweka sawa katika mwonekano.
Kwa upande wake, Jack
aliwashauri warembo wengine kuvikimbia vyakula vinavyosababisha mwili
‘kuumuka’ na kupoteza mwonekano mzuri.
JACK MAISHA PLUS, RUBI WAFANYA MAZOEZI KUONDOA ‘VITAMBI’

