Kufuatia uvumi kuwa P Square wanamiliki Private Jet wakali hao wameamua
kuvunja ukimya na kuzungumzia tetesi hizo wakikanusha kuwa si kweli.
P Square wamesema kwamba kilichopo nimakubaliano na kampuni fulani ya
Private Jet kutumia ndege hiyo kwenye safari zao kwasababu inarahisisha
mambo mengi.
Hata hivyo wakali hao wamefafanua kuwa kukodi private Jet hakuna
maana kuwa hawana uwezo wa kununua ya kwao kwasababu hata sasa wanapanga
kununua Jet yao binafsi maalumu kwa safari zao.
Aidha Wakali hao wameongela kusikitishwa kwao baada ya kusikia habari za kufungiwa kwa single yao ya Alingo.
“Tumeskia kuhusu kukatazwa wimbo wa Alingo, lakini hatujapewa sababu
za msingi kwanini imefikia hatua hiyo. Tulichogundua ambacho hawajui ni
kwamba unapoufungia wimbo unaufanya upate umaarufu haraka, na kukataza
wimbo kwenye channel Nigeria si jambo la msingi kwasababu channel za
kimataifa wanaendelea kuupiga”. Alisema Peter
BAADA YA KUONEKANA WAKIWA NDANI YA PRIVATE JET, P SQUARE WAFUNGUKA!

