Wanawake wawili kutoka mji wa Kiambu, Central Province, Kenya walibambwa
na walinzi wa supermarket wiki iliyopita, wakiwa na lita tano za mafuta
ya kupikia kati ya mapaja yao. Wanawake hao, inasemekana ni baadhi ya
wahusika katika genge maarufu la uibaji madukani (shop lifting)
kwa mujibu wa utawala wa supermarket hiyo, wamekua wakiibiwa sana,
kitu kilichowalazimu kuweka video camera ya ulinzi (CCTV) ili kupunguza
wizi huo. Miezi michache tu iliyopita, mwanamke aliyevaa baibui
alikamatwa na bidhaa zenye thamani ya maelfu ya shilingi (Kenyan
shillings) akiwa amezificha ndani ya nguo zake.
Wanawake hawa
wawili, siku yao ya arobaini iliwadia walipoamriwa warudi ndani na
walinzi wakati wakijaribu kuondoka kutoka kwenye supermarket hiyo.
Walijaribu kujikausha ili wasishtukiwe lakini ilikua too late maana
walinzi walishajua wanawake hao wana vitu gani kati ya mapaja yao.
Walikamatwa
na kufungwa kamba kama mbuzi kwenye lango la kuingilia kwenye
supermarket hiyo, na kulazimishwa kufunua sketi zao ili walichoiba
kionekane kwa watu wote wanaoingia kwenye supermarket hiyo.
Haijajulikana kama dhumuni lilikua kuwaaibisha, kuitaarifu jamii kwamba
hawa ni wezi, kutoa fundisho kwa vibaka wengine, au vyote. Walishikiliwa
hapo mpaka polisi walipowasili na kuwachukua.
BALAA:WANAWAKE WEZI WANASWA SUPERMARKET WAKIIBA BIDHAA NA KUFICHA KWENYE TUPU ZAO(SEHEMU ZA SIRI)....!

