Habari mpya kitaa kwasasa ni kwamba Queen wa Bongomovie Wema Sepetu
amemsign Kajala kufanya kazi chini ya uangalizi wa kampuni yake ya
Endless Fame.
Wema amesema kwamba hadi kufikia sasa Kajala anafanyia kazi Script ya
filamu yake mpya inayoitwa ‘Princess Sasha’ ambayo tayari imeshaanza
kumulikwa na huenda kazi yote ikamalizika siku ya jumalipili.
Aidha kufuatia uvumi kuwa Wema anamtumia Shostisto wake Kajala kurudisha
kiasi cha pesa alichogharamia katika dhamana yake Star huyo amekanusha
vikali na kusema kwamba hakuna ukweli dhidi ya tetesi hizo.
Wema amesema amemsign kajala kama actress mkali ambae anaamini
kiwango chake kizuri katika kazi za uigizaji na kuongeza kuwa hata sasa
watakapofanya kazi ya kufyatua filamu atamlipa kama ambavyo angefanya
kwa msanii mwingine.
Star huyo amesema kuwa filamu ya ‘Princess Sasha’ itakuwa inahusu
story ya mtoto wa mfalme nafasi ambayo itachezwa na kajala akiwa kama
main character na kutakuwa na mambo mengi yakuvutia ambayo yatatokezea
baadae kwenye hadithi ya filamu hiyo.
WEMA AMSAINISHA KAJALA ENDLESS FAME....SOMA ZAIDI HAAPA

