BIASHARA ya ngono katika mji wa Dodoma
imeshika kasi kubwa ambapo imebainika kuwa wateja wakubwa ni watumishi
wa serikali, wanasiasa na madereva.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa katika biashara hiyo kuna
makundi mbalimbali yanayotofautiana kwa malipo ya biashara hiyo.
Wapo
wanafunzi wa vyuo vikuu na wanawake ambao wamedai kuwa wanalazimika
kufanya biashara hiyo kutokana na kubanwa na maisha, hususani katika
marejesho ya mikopo wanaichukua kutoka katika taasisi mbalimbali ya
kifedha.
Mmoja
wa wafanyabiashara ya ngono (jina tunalo) bila kujua anaongea na nani,
alieleza kuwa kwa sasa katika mji wa Dodoma kuna ushindani mkubwa wa
biashara ya ngono kwani wanafunzi wa vyuo vikuu vya mjini hapa vimeteka
soko hilo.
Alisema kutokana na ushindani huo kwa sasa kima cha chini ni sh 7,000 kwa mchepuo mmoja na sh 30,000 hadi 40,000 kwa kulala.
Mfanyabiashara
huyo alieleza kuwa wateja wakubwa wa ngono ni wafanyakazi wa serikali,
wanasiasa (wabunge), madereva pamoja na wafanyakazi wa benki.
Bila
hofu mfanyabiashara huyo alieleza kuwa kuanzia muda wa saa tatu hadi
sita usiku wanajipanga katika maeneo ya biashara na yanapofika magari
hujipanga mbele ya gari ili mteja amchague anayemtaka.
“Hapa
tupo wengi, lakini pia wengine ni wafanyakazi wa serikali wanakuja
hapa kujiuza, wanafunzi wa vyuo vikuu nao hivyo hivyo… Mimi nipo hapa
ninakuja kwa siku maalum ambazo ninakuwa nimekwama.
“Ninakabiliwa
na masuala ya mikopo. Unajua hapa tupo kama kumi akina mama ambao
tumekopa mikopo katika taasisi mbalimbali, lakini mitaji inapoyumba
unajiuliza utapata wapi, unalazimika kuja kufanya biashara,” alisema.
Aliongeza
kuwa kwa kawaida mtu mmoja anaweza kufanya ngono na watu wasiopungua
saba kwa siku, hivyo ana uhakika wa kujipatia kiasi cha sh 70,000 iwapo
siku itakuwa nzuri.
Alibainisha
kuwa na kama siku ni mbaya anaweza kupata kiasi cha sh 49,000 iwapo
atalipwa sh 7,000 kwa mchepuo mmoja.
Uchunguzi wa kina uliofanyika
umebaini maeneo ambayo yana wasichana wengi ambao ni makahaba ni Chako
Nichako, Double H na Mtaa wa Uhindini ambako kuna gesti maarufu kwa
kufanya biashara hiyo.
Hata hivyo, imebainika kuwa makahaba wa vyuo vikuu viwango vyao ni kuanzia sh 200,000 kulala na sh 30,000 kwa mchepuo mmoja.
Mmoja
wa waendesha bodaboda ambaye hakutaka jina lake litajwe, alieleza kuwa
katika biashara hiyo yapo maeneo ambayo kwa sasa kuna wakala wenye
kundi kubwa la wasichana anaowauza.
Wakati
biashara ya ngono ikionekana kushamiri, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rehema
Nchimbi alishatangaza kuwawinda na kuwatia kwenye mikono ya sheria
wale wanaojihusisha nayo.
Hata hivyo, kauli hiyo inaonekana kukosa mashiko kwani biashara hiyo inazidi kushamiri siku hadi siku.
BIASHARA YA NGONO YAZIDI KUSHAMIRI DODOMA.....MAKAHABA WA DAR NAO WACHACHAMAA NA KUPIGA KAMBI

