Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ, limekanusha taarifa
zilizotapakaa kwenye mitandao kuwa askari wa jeshi hilo waliokwenda huko
kwa ajili ya kulinda amani,wameanza kujihusisha na makahaba.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Mtandao wa
www.congodrcnews.com umedai wanajeshi wa Tanzania wameanza kujihusisha na
ubakaji wanawake katika Mji wa Sake ulioko Goma.
Taarifa hizo
zimeeleza kuwa askari mmoja wa JWTZ alihitaji kujamiiana na mwanamke
mmoja(Kahaba) kwa ujira wa Dola 50. Baada ya kumaliza shida zake ambazo
ilielezwa alizifanya bila kinga yoyote,askari huyo alikataa kumlipa
ujira wake,hali iliyoleta tafrani na mwanamke huyo kupiga kelele.
“JWTZ
linapenda kuwaeleza wananchi kuwa taarifa hizo ni za uongo mtupu wenye
nia ya kulipaka matope JWTZ na Tanzania kwa ujumla. “Picha iliyotolewa
kwenye tovuti hiyo ya www.congodrcnews.com ni ya wanajeshi wa Tanzania
walipokuwa katika Operesheni ya huko Comoro mwaka 2008.
Mtu anayeonekana kuwa chini ya Ulinzi alikuwa ni mshiriki wa Kanali Mohamed Bacar ambaye aliondolewa madarakani.
“Vilevile picha hiyo ilitolewa vile vile katika tovuti za www.apc.net.au/news/stories ya Machi 26, 2008 na ww.Seattletimes.com.
na pia picha hiyo ipo pia kwenye tovuti ya Jamii Forum baada ya kufanya
‘link’ kutoka kwenye Mtando wa www.google.com.”
Taarifa hiyo
ilisema kuwa JWTZ inapenda kueleza wananchi na dunia kwa ujumla kwamba
wanaoneza taarifa hizo wana lengo la kukatisha tamaa juhudi zinazofanywa
na nchi za Maziwa Makuu na SADC kuleta amani nchini DRC kwani
JWTZ wako DRC kwa mujibu wa taratibu za kiutendaji za Umoja wa
Mataifa.
JWTZ YABEZA TAARIFA ZA ASKARI WAKE KUJIHUSISHA NA "BIASHARA YA KUKUNUA MALAYA " HUKO CONGO

