skip to main |
skip to sidebar

10:58 AM

Anonymous
JB bonge la bwana mwigizaji wa filamu Swahiliwood
MWIGIZAJI mahiri wa filamu Bongo Jacob Stephen ‘JB’ amedai kuwa mwili
wake umekuwa gumzo hata mwenyewe anakereka kwa kuongelewa kama bonge
hata watu kuhisi kama labda unampata shida katika kutembea au ni mtu
asiye na mazoezi kumbe yeye ni mwepesi kama Messi mchezaji wa mpira wa
Barcelona fc ambaye anaweza kupenya ngome yoyote ya wapinzani.
.
JB Bonge la Bwana akiwa na mwigizaji Stara.
“Ni kweli kuna wakati nahitaji kufanya mazoezi lakini tatizo si
mazoezi kwangu unene huu ni kwa sababu moja tu kula sana chakula kingi
kila wakati nakula sana nahisi hata Oxfam hawakukosea kunipa ubalozi wa
chakula ni sehemu ambayo nastaili napenda sana kula kula vyakula na ndio
huu unene unao uona sasa,”anasema JB.
JB mwigizaji bora anayetamba na filamu zinazotikisa kwa sasa za
Nakwenda kwa Mwanangu na Zawadi yangu, anasema kuna wakati unene
unamtesa sana na kutamani apungue kwani unene huo unamtesa hasa katika
mavazi, kwa sababu mavazi anayovaa kwa sasa anaagiza kutoka nje ya Nchi
baada ya kutuma vipimo hivyo kama anahitaji nguo haraka ni vigumu kufika
kwa wakati hiyo inatokana na kukosa mafundi au wabunifu wa hapa nchini.