10. Kala Jeremiah Kusaini Mkataba na pepsi
Kala Jeremiah msanii mwenye tunzo 3 za hip hop kutoka Kili Music
Award 2013alisaini mkataba wa miezi 6 kutoka kampuni ya PEPSI kama
balozi wa soda hiyo. Kala alisema mkataba huo umempa furaha sana na
amejisikia faraja sana. Sasa kala anaonekana kwenye matangazo ya pepsi
na ni kitu cha kufurahisha kwenye muziki wetu.tutegemee mambo makubwa
kutoka kwa kala mwaka ujao.

09 . Mabeste , Vanessa Mdee , Gosby Kuondoka BHITS
Hii ni kitu ambacho kilizua utata sana na mshangao baina ya wapenzi
wa bongoflava. Mabeste ndio alikua wakwanza kutangaza hayupo BHITS
“Tatizo ni maelewano ya kibiashara kati ya mimi na uwongozi wa B”hits na
si vinginevyo…..!! Akuna mtu ambaye apendi kuona faida kwenye kazi
yake…!! Na kwasababu music ni kazi …Baaasi nimejaribu kutetea kazi
yangu…!! Pamoja saana” alisema mabeste. Vamessa na Gosby hawakuweza
kuzungumzia kwa undani kuhusiana na hali hii.

08 . P-Square in Dar
” Eh – I no go lie , The things wey dey my mind , When I see you
dancing, girl you got me high , And if you want to try, Gbege go dey
tonight , Cos I’m in the mood , As long as you feeling the groove , I
go deal with you , Personally eh ,Personal personally – ah ah ah a ,
Personally eh…. ” hii ndio ilikua anthem mwaka huu na pale leaders club
ambapo psuare walidondosha shoo moja ya kufa mtu.


07. Emmanuel msuya wins Epiq Bongo Star Search
Ni mashindano yaliyokua yamejaa ushindani mkubwa sana kwa mwaka huu
hasa kwa upande wa kina dada baada ya wanne kati ya 5 kufanikiwa kuingia
katika top 5 lakini hiyo hakuhakikishia kwamba ushindi utabaki kwao
kwani emmanuel msuya alifanikiwa kuwabwaga wote usiku wa kuamkia leo
pale escape one na kitwaa taji la mshindi wa EBSS kwa mwaka huu, taji
ambalo lilikua linashikiliwa na walter chilambo.

06 . AY awa nominated 2 times kwenye Channel O Music Awards
Kwa mwaka wa pili sasa AY ameweza kumaintain nominations zake katika
tuzo za channel o lakini cha tofauti na mwaa 2012 ni kwamba mwaka huu AY
alikua nominated lakini hakupata tuzo . Hii haimshushi AY sababu kuwa
recognized Africa ni jambo kubwa kwani kuna wasanii wakubwa sana hapa
Tanzania kuliko AY lakini hatuwaoni kwenye tuzo kama hizi.

05 . Barack Obama Amfollow Vanessa Mdee Twitter
moja ya vitu ambavyo watanzania tunajivunia ni uhusiano wetu mzuri na
nchi ya marekani hasa raisi wa sasa barack obama na hata aliyepita
george bush.barack obama alivyodondoka kutoka state na kuja kukutembelea
hapa tanzania. moja ya kitu ambacho obama alishangwazwa nacho ni
mapokezi aliyoyapata alivyokuja Tanzania na hii sasa tunaona imeanza
kuzaa matunda baada ya obama kumfollow vanessa mdee kwenye ukurasa wake
wa twitter.

04 . Diamond na Lady Jay dee Kuchukuliwa na Coke Studio
Coke Studio mwaka huu walifika africa ikiwa ni project iliyokwisha
kufanyika baadhi ya nchi kama Brazil na India. Kwa upande wa Bongo
Tulifanikiwa kuwaona manguli wawili wamuziki wa bongo flava namaanisha
King Diamond Platnumz ambae hana dalili za kuachia his crown na Queen
Lady jay dee wakiperform nyimbo mbalimbali. Hii imekua njia nzuri sana
ya kuutangaza muziki wa bongo Africa na ni moja ya Breakthrough ya
muziki kwa mwaka huu.

03 . Adam Juma Kuacha Kufanya Music Videos
Unaweza kujiuliza kwa nini huoni video kali za Adam Juma
katika soko mtu tuliemzoea katika Industry baada ya kuletea mapinduzi
makubwa sana katika sanaa mpaka kufikia level ya Tzee kuweza kushindana
na mataifa mengine ya Afrika.Adam Juma despite na kazi yote aliyoifanya
katika muziki but still haikuweza kumlipa kiivyo na akaamua kufanya
maamuzi magumu ya kukaa pembezi kwa muda akijipanga tena na kwasasa
amejikita sana katika kufanya video za documentary na matangazo.

02. Diamond Platnumz na Number One Movement
Baada ya adam juma kuondoka katika video productions diamond aliamua
kufanya kitu ambacho hamna mtu alishawahi kukifanya, alichomoa milioni
45 na kudondoka africa kusini kufanya tunachoweza kusema video kali
kuliko zote kwa hapa bongo na sio tu kwa mwaka huu bali tokea muziki huu
wa bongo flava ulipoanza. Chakutegemea mwaka 2014 ni revoultion zaidi
katika ulimwengu wa video hasa kama alivyosema diamond mwenyewe kuwa
pesa alizotumia katika video hii ilikua ni kama investment kwasababu
mwishoo wa siku mziki unalipa siku hizi sio kama zamani so pesa zote
zinakuja kurudi baadae.

01. Kifo Cha Albert Mangwair
Kama wewe sio mpenzi wa bongo movies sana basi inawezekana kifo cha
ngwea ndio kikawa kimekuuma zaidi. jamaa ni moja ya vichwa vya mistari
na mashairi vilivyokua vimebaki. ngwea alifariki akiwa na miaka 31 tu na
muziki kwake ulikua bado haujafa. Ngwea alifariki akiwa chumbani
huko afrika ya kusini ambapo asubuhi kulipokucha jamaa alikua amelala
fofofo, rafiki zake wakajaribu kumwamsha na kumwagia maji bila mafaniko
ndo ikabidi wamwahishe hospitali ya St. Hellen ya jijini Johanesburg
ambapo madaktari walijaribu kuokoa maisha yake bila mafanikio, ndipo
madaktari wakatoa ripoti kuwa msanii huyo ameaga dunia.

Imeandikwa na VIBER