

NDOA ya Rais Barak Obama na mkewe Michelle haitaweza kuvunjika kwa sasa kwa vile mke huyo mrembo atatakiwa kuendelea kuishi katika Ikulu ya White House hadi mumewe atakapomaliza muhula wake wa pili wa uongozi mwaka 2016.


...Akifurahia jambo wakati mkewe kanuna.
Juzi, Gazeti la The Nation la Marekani liliripoti kuparaganyika kwa
ndoa hiyo iliyowahi kutajwa kama ndiyo bora zaidi duniani, kwa kile
kilichoelezwa kuwa kuchukia kwa Michelle baada ya kumwona mumewe
akishoboka na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt wakati wa
shughuli za kumuaga rais wa zamani wa Afrika Kusini, hayati Nelson
Mandela ‘Madiba’.

Helle akimuonyesha kitu Obama.
Mwaka 2012, uvumi ulisambaa kwa kasi duniani ukielezea kutengana kwa
watu hao wawili maarufu zaidi, hali iliyosababisha Ikulu ya Marekani
kukanusha taarifa hizo.
Hata hivyo, hadi gazeti hili linakwenda
mitamboni, hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na ikulu, Obama wala
Michelle juu ya madai ya kutengana kwao.

