Alichofanyiwa Kimwana Manywele, Halima Haroun kwenye ‘bethidei’
yake kimetafsiriwa kuwa ni sawa na kumkufuru Mungu baada ya baadhi ya
wageni waalikwa akiwemo Nasibu Abdul ‘Diamond’ kutumia juisi, maji na
soda kumuogesha.
Ishu hiyo ilichukua nafasi ndani ya Hoteli ya
Demage, Mwananyamala jijini Dar ambapo
mwanadada huyo akiwalisha keki wageni waalikwa na baada ya zoezi hilo,
watu walimvaa na kuanza kummiminia kichwani vinywaji hivyo na kumlowesha
mwili mzima.
Kitendo hicho mbali na kulinogesha tukio hilo, wapo
walio laani wakisema kuwa, tabia hiyo si nzuri kwani kutumia vinywaji
kumuogesha mtu wakati kuna wanaovitafuta bila kuvipata ni sawa na
kumkufuru Mungu.
“Dhambi iliyoje, watu wanatumia vinywaji kuogeshea
mtu? Kuna faida gani sasa kufanya hivyo? Kama wana pesa zisizo na kazi ni bora wakawape masikini wanaoshinda na njaa kuliko kufanya vile?” alihoji
Jumaa Shemputa wa Kinondoni jijini Dar.
'HAPPYBIRTHDAY’ YA HALIMA, BALAA....

