Shilole na mwimbaji wa Kofi.
Msanii wa sinema na muziki wa Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Desemba
16, mwaka huu alinaswa gizani akiwa amejiweka kimahaba kwa mmoja wa
waimbaji wa mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),
Antoine Christophe Agbepa Mumba ‘Koffi Olomide’, Ijumaa lilimbamba.
Tukio hilo lilitokea ndani ya Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini
Dar, ambapo Shilole alienda kwa ajili ya kushuhudia shoo ya mwanamuziki
huyo.
Akiwa ndani ya viwanja hivyo, Shilole alijikuta akishobokewa
na mmoja wa wanamuziki wa Koffi ambaye jina lake halikupatikana mara
moja ambapo kuna muda wawili hao walikutwa nyuma ya jukwaa jamaa
‘akiimbisha’.
Haikuweza kufahamika mara moja kama Shilole alimkubalia mshikaji huyo
lakini wadakuzi wanadai baada ya shoo kumalizika, mwanamuziki huyo
alimfuta tena Shilole na kuongozana naye hadi kwenye gari alilokwenda
nalo pale ukumbini.
SHILOLE NA MWIMBAJI WA KOFI OLOMIDE WANASWA GIZANI

