Mtoto wa ajabu aliyezaliwa na mwanamke Emeliana Wilson mkoani Mbeya hivi karibuni.
Mmoja wa watu waliyomuona mtoto huyo aliyezaliwa akiwa na macho
yaliyoungana, kitu kama pembe katika paji la uso wake na kutokuwa na pua
alisema yawezekana kuna mambo ya Kiswahili nyuma ya tukio hilo.
“Huyo
mtoto siyo bure, yawezekana mama yake amekwenda kinyume na taratibu
anazotakiwa kuzifuata mama mjamzito. Pia huenda kuna watu wabaya
wameamua ‘kumchezea’ mama wa watu ili ajifungue mtoto wa ajabu kwa sababu
wanazozijua wao,” alidai shuhuda huyo.
Mama wa mtoto huyo akizungumza
na mwandishi wa habari wa gazeti moja litokalo kila siku alikiri kupata ujazito wa mtoto huyo baada ya kwenda kwa mganga
wa jadi na kupewa dawa za miti shamba.
Aidha, mama huyo ameomba
msaada kutoka kwa wasamaria wema wa kumuwezesha kumlea mwanaye kwa madai
kwamba mumewe, Emmanuel Mbukwa ametoweka baada ya kumuona mtoto huyo wa
ajabu.
USHIRIKINA WAHUSISHWA UZAWA WA MTOTO WA AJABU.

