Mwanamuziki wa Uganda , Jose Chameleone anaweza kujikuta akikabiliwa
na kesi ya mauaji kutokana na kifo cha kijana mwenye miaka 27, Robert
Karamagi aliyefariki hospitali baada ya kujichoma moto nyumbani kwa
mwanamuziki huyo.
Joseph Mayanja na mke wake Daniella Atim Mayanja na wengine wanaoishi
nyumbani kwake wanafikiriwa na polisi kuhusu kushtakiwa kwa kifo
Karamagi.
Ripoti za awali zinadai kuwa Karamagi alijaribu kupora nyumbani kwa
Chameleone lakini alikuwa na nia ya kumuua Daniella. Hata hivyo kwa
bahati mbaya alijichoma moto mwenyewe uliomsababishia majeraha na
hatimaye kifo.
Daniela (mke wa Chameleone)
Baba yake amezikataa taarifa kuwa mwanae alijichoma moto na kudai
kuwa alimpigia akiwa hospitali kumwambia kuwa Chameleone na washkaji
zake walimpiga, kumtesa na kumchoma moto.
CHAMELEONI NDANI YA MTEGO MZITO.....YAWEZEKANA AKASHITAKIWA KWA KOSA LA MAUAJI

