
MSANII nyota wa miondoko ya Mchiriku, Omari Omari,
aliyefariki leo afajiri atazikwa kesho saa 7 mchana. Kwa mujibu wa King
Sapeto, rafiki wa karibu wa marehemu, mazishi yatafanyika Temeke
Mikoroshini jijin iDar es Salaam na kuanzia leo ndugu na jamaa wa
marehemu wanategemea ujumbe mzito kutoka kwa viongozi wa Serikali
watakaopishana kwenda kutoa mkono wa faraja kwenye nyumba ya msiba.
Kwa
siku za hivi karibuni viongozi wa serikali na vyama mbali mbali vya
siasa wamekuwa mstari wa mbele kwa kushiriki bega kwa bega kwenye
misiba ya wasanii, hivyo watu wa karibu na Omari Omari wanategemea hali
hiyo pia itatokea kwa ndugu yao kipenzi. "Hatutegemi ubaguzi wa misiba"
anaeleza mmoja wa ndugu wa marehemu.
Omari
Omari aliyetamba na wimbo “Kupata Majaaliwa” ndani yake kukiwa na
mstari mkali unaosema ndefu amekosa ng’ombe lakini mbuzi kapewa,
alifariki katika hospitali kuu ya Temeke baada ya kuugua ugonjwa wa
kifua kikuu.
Msiba uko Temeke Mikoroshini nyumbani kwa baba yake.
MUNGU AMLAZE MAHALA PEMBA PEPONI- AMINA