Mganga
wa jadi almaarufu sangoma aliyetajwa kwa jina la Wadebi Jinasa amepata
aibu ya karne baada ya kunaswa ‘live’ na wake za watu kwenye gesti moja
(jina linahifadhiwa) iliyopo Tandika jijini Dar es Salaam.
Tukio
hilo la aina yake lilijiri maeneo hayo, usiku wa manane wa kuamkia
Jumanne iliyopita, wakati waumini wa Dini ya Kiislamu waliofunga kwa
ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakila daku.
Kwa
mujibu wa mashuhuda, jamaa huyo alidaiwa kuwa alikuwa akiwafanyia wake
hao wa watu dawa ya mapenzi kwa kuwavua nguo zote kisha ‘kuwachezea’.
Mume na Mke wakizozana.
Ilidaiwa kuwa mbali na kuwachezea, amekuwa akiwafanyia mchezo usiofaa mmoja baada ya mwingine.
Chanzo cha sakata hilo kilidai kuwa sangoma huyo amekuwa na tabia hiyo hasa akimuona mwanamke mwenye mvuto katika hali ambayo haikueleweka mara moja humuita majina yake matatu, yaani la kwake, baba hadi la babu yake, jambo linalosababisha anayeitwa kushtuka na kuhisi mtu huyo atakuwa anamfahamu kiundani.

Ilidaiwa
kuwa baada ya mwanamke huyo kusimama huanza kumwelezea matatizo yake na
kumtajiwa hadi matatizo yanayowapata ndugu zake walio vijijini na
sehemu nyingine za mbali.
Kiliendelea
kudai kwamba, sangoma huyo amekuwa akiwavuta wanawake wengi kwa
kuwatajia matatizo yao sawia bila kukosea hivyo kuwachanganya na
kumjengea imani kuwa ni ‘fundi’ wa masuala hayo.
Kufuatia
vituko vyake, juzikati mume wa mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa),
Huruka Hassan alirejea nyumbani kwake na kukuta mkewe hayupo.Alidai
alipofanya uchunguzi wa haraka, aligundua ameenda kwenye gesti hiyo
kupata tiba.
Ilidaiwa kwamba, siku zote Huruka amekuwa akimuacha mkewe akapate tiba lakini siku ya tukio machale yalimcheza, alipofika kwenye gesti hiyo alijibanza ukumbini na kusikia sauti ya mkewe ikinong’ona chumbani na sauti ya ‘besi’ la sangoma huyo kwa mbaaali.
Sangoma akiwa na mawazo baada ya kunaswa.
Ilidaiwa kwamba, siku zote Huruka amekuwa akimuacha mkewe akapate tiba lakini siku ya tukio machale yalimcheza, alipofika kwenye gesti hiyo alijibanza ukumbini na kusikia sauti ya mkewe ikinong’ona chumbani na sauti ya ‘besi’ la sangoma huyo kwa mbaaali.
Ilisemekana
kwamba uzalendo ulimshinda Huruka na kujikuta akivunja masharti ya
kilinge cha sangoma huyo kwa kuchungulia kwenye tundu la kupitisha
funguo.
“Haaamadi!” alisikika Huruka alimuona laivu mkewe akiwa mtupu akitaka kufanyiwa vitendo vichafu ambapo sangoma huyo alidaiwa kuwa alikuwa akjiandaa kumfanyia ‘amshaamsha’.
“Haaamadi!” alisikika Huruka alimuona laivu mkewe akiwa mtupu akitaka kufanyiwa vitendo vichafu ambapo sangoma huyo alidaiwa kuwa alikuwa akjiandaa kumfanyia ‘amshaamsha’.
Ilidaiwa
kuwa Huruka alishindwa kujizuia, akagonga mlango kwa hasira ambapo
sangoma alivaa ‘chapchap’ na kufungua.Ilielezwa kwamba walipokutana uso
kwa uso, Huruka alitunishiana misuli na sangoma huyo wakataka kuzichapa
lakini jamaa akaona amchukue mkewe na kutimka naye.
Baada
ya mke wa Huruka kuokolewa kufanyiwa ukenge, mwanaume mwingine wa eneo
hilo, Tabu Abdallah naye alidai kumnasa mkewe kwenye gesti hiyo akiwa
amekalishwa kama alivyozaliwa, akitolewa vitu fulani tumboni na sangoma
huyo.
Akizungumza
na mwanahabari wetu aliyekuwepo eneo la tukio usiku huo, Tabu alisema
alimnasa mkewe na sangoma huyo baada ya kutonywa juu ya mkewe kuingia
gesti hiyo.
Alisema sangoma huyo alimchukua mkewe kwa gia ya kumtibia kumbe alikuwa na lake jambo.
Baada
ya kutokea kwa mtiti huo, Mjumbe wa Shina namba 29, Azimio-Tandika,
Faraj Neto, wanawake waliodhalilishwa, waume zao, polisi na mmliki wa
gesti hiyo, Ebenezer Ngowo, walimchomoa sangoma huyo kwenye gesti hiyo.
Katika
hali ya kushangaza mke wa Tabu alikuwa akimlaumu mumewe kwa kutaka
kumpiga mganga wake ambaye alikuwa akitaka kummalizia matatizo huku
wanawake wengine wakiwaomba radhi waume zao na kudai walirubuniwa.
Akizungumizia
mkasa huo mke wa Tabu alisema kuna siku alikutana na mganga huyo njiani
ambapo alimwita majina yake matatu, aliposimama kumsikiliza ndiyo
akaanza kumtajia matatizo yake, jina la mama yake mzazi na kumwambia
mama huyo huko aliko ana tatizo sugu la miguu jambo ambalo ni kweli
ndipo alianza kumuamini.
MWISHO WA SAKATA
Mwisho wa sakata hilo, mjumbe wa nyumba kumi alimtaka sangoma huyo
kuondoka eneo hilo na mmiliki wa gesti hiyo alimtaka mganga huyo kuhama
kwenye gesti yake kutokana na tabia yake ya kubadilisha wanawake.
Kwa upande wao, polisi walimshikilia sangoma huyo kutokana na sababu za
kiusalama kufuatia wenye wake na wananchi wenye hasira kutaka kumpiga
mawe na kumuua.