“Kawaida ya Shilole jukwaani huwa habahatishi na niwaambie tu utakuwa mchuano mkubwa siku hiyo kwani hapa Shilole pale Yemi Alade, sijui nani ataibuka kidedea wa shoo siku hiyo, mashabiki wenyewe ndiyo watakaoamua,” alisema Maloto.
Utamu wa tamasha hilo hautaishia hapo, Maloto alisema watakuwepo pia waimbaji wanaotamba kunako muziki wa Injili ambao watatoa burudani nzuri ya kumsifu Mungu.
“Listi ni ndefu na inazidi kuongezeka kila kukicha na mpaka sasa wasanii wakubwa wa muziki wa Injili tutakaokuwa nao ni pamoja na Upendo Nkone, Ambwene Mwasongwe, Angela, Paul Clement na Martha Mwaipaja,” alisema Maloto.
Maloto alisema, katika eneo la Bongo Fleva, watakuwepo wasanii lukuki kulipamba tamasha hilo kwa kiingilio cha shilingi elfu tano tu.“Bado wasanii wanaendelea kuongezeka lakini hadi sasa tumeshawaweka mkononi Madee, R.O.M.A Mkatoliki, Meninah, Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi, Ali Kiba na kwa mara ya kwanza Wema Sepetu atapanda jukwaani na kuimba nyimbo za bebi wake Diamond,” alisema Maloto.
“Tutakuwa na mwanamuziki Khalid Chokoraa ambaye atazichapa ulingoni na Said Memba huku Bingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Thomas Mashali akizitwanga na ‘mbunge mtarajiwa’, Mada Maugo.
“Ushindani mkali pia utawekwa na mastaa wa Bongo Movie, Cloud 112 na Jacob Steven ‘JB’ ambao siku hiyo watazipiga katika pambano la raundi 4,” alisema Maloto.
Maloto alimaliza kwa kusema kuwa kutakuwa na mechi kali kati ya Wabunge Mashabiki wa Yanga dhidi ya wenzao wa Simba huku timu ya Bongo Movie ikiingia uwanjani kumenyana na Bongo Movie.
Tamasha hilo limedhaminiwa na kampuni ya Vodacom, Pepsi, Azam TV, EFM (93.7), Clouds FM (88.5), Sycorp pamoja na Times FM (100.5).