LULU: MNAIBIWA BURE, MIMI SIPO FB


STAA wa filamu Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema hajawahi kufungua akaunti kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook ‘FB’ na kwamba aliyefungua kwa jina lake ana nia ya kuwaibia mashabiki wake.
Staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumzia akaunti hiyo inayoonekana ni feki yenye sura ya kuwaingiza mjini mashabiki wake, Lulu alisema haitambui na wanaokubali kujiunga na ‘Lulu’ huyo wanataka kuibiwa.
“Hee nashangaa kwa kweli, yaani sielewi chochote kuhusu akaunti hiyo, sina akauti Facebook nashangaa sana kwa hilo swala wasitake kunichafulia,” alisema Lulu.


Twitter Delicious Facebook Digg Favorites More