MWANADADA anayefanya vizuri katika soko la filamu Bongo, Jacqueline Wolper amejitapa kuwa amejipanga vizuri katika kuhakikisha kuwa, siku ya tamasha kubwa la Usiku wa Matumaini atafanya mambo makubwa.
“Nipo katika maandalizi makubwa sana, sasa hivi naendelea na mazoezi ya kawaida wakati namsubiri mwalimu wangu ambaye naamini atanipa mbinu za kumkalisha chini mpinzani wangu,” alisema Wolper.