Staa wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema kuwa
anapokuwa nyumbani kwao marafiki zake wakubwa ni mbwa wake wawili ambao
anawafuga kwa sasa.
Akiongea kwa kujiamini, Johari alisema kuwa mbwa hao huwa
wanamsaidia pindi anapokuwa na mawazo kwani humchangamsha pale
anapocheza nao.
“Unajua nawapenda sana mbwa wangu na sijui ni kwa
nini nilichelewa sana kuwatafuta, mara nyingi hunifariji wakati
ninapokuwa na mawazo mabaya,” alisema Johari.
Mbali na mbwa hao, pia
Johari alisema kuwa siku mojamoja huenda kuchungulia katika bendi
mbalimbali za burudani kwa ajili ya kuchangamsha akili yake.
JOHARI ADAI MBWA WAKE HUMUONDOLEA MAWAZO NA KUMFARIJI

