Gari aina ya Toyota Starlet
lenye namba za usajili T 382 BUN likiteketea kwa moto nje kidogo ya
ofisi za Mkuu wa Mkoa, Ilala Boma jijini Dar es Salaam.
Gari aina ya Toyota Starlet
lenye namba za usajili T 382 BUN mali ya mwanamke mmoja ambaye hakutaka
kutaja jina lake, limeteketea kwa moto nje kidogo ya ofisi za
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam zilizopo Ilala - Boma. Kitendo cha ajabu
ni kuona vijana waliokuwa eneo hilo baada ya kusaidia kuzima moto
usiendelee kuliteketeza gari hilo, walionekana wakiwa 'busy' kung'oa
baadhi ya spea za gari hilo.
Baadhi ya vijana wa eneo hilo wakijaribu kuiba baadhi ya spea za gari hilo wakati likiungua.
GARI LATEKETEA KWA MOTO NJE YA OFISI ZA MKUU WA MKOA ILALA JIJINI DAR

