Aliyekua mtangazaji wa Runinga ya C2C ambaye kwa sasa ni mwigizaji,
Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’, ametoa kali baada ya kufunguka kuwa
siku akiamka asubuhi na kukuta makalio yake hayapo, atakimbilia kwa
mchungaji akafanyiwe maombi.
Akizungumza na paparazi , mtangazaji huyo
ambaye ana vituko lukuki, alisema kila siku anapoamka asubuhi, lazima
aangalie kama makalio yake yapo ndiyo mambo mengine yafuatie.
“Jamani nikiamka kitandani, kabla ya kuoga na kupiga mswaki cha kwanza
najitazama nyuma kama hili nililojaliwa na Mungu lipo na nisipolikuta,
nakimbilia kwa mchungaji kuombewa fasta,” alisema Lulu.
Lulu
aliongeza kuwa, hakuna kitu anachokipenda katika mwili kama makalio
yake, hivyo hayupo tayari kuishi bila ya hayo makalio kwani ndiyo kila
kitu katika mwili wake.
“Haya ndiyo kila kitu, usiniulize kwa nini nayapenda sababu naijua mimi mwenyewe,” alisema.
NIKIKUTA MAKALIO HAYAPO, NAENDA KWA MCHUNGAJI

