MISS Temeke 2006/07 mwenye ‘taito’ kibao Bongo, Jokate Mwegelo anadaiwa
kuchumbiwa kwa siri nyumbani kwao, Songea mkoani Ruvuma alipokwenda
kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya, Ijumaa Wikienda limenyetishiwa.

Jokate Mwegelo.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa staa huyo, Jokate alitimba Songea akiongozana na rafiki zake wawili pamoja na baadhi ya ndugu.Chanzo hicho kilidai kuwa kilipochunguza amekwenda kufanya nini mkoani humo, ndipo ikabainika kuwa alikwenda kusherehekea Mwaka Mpya akiongozana na wazazi wake anaoishi nao Dar, lengo likiwa kukamilisha mambo ya mila kwani alikuwa ameposwa na mchumba ambaye hakutajwa.
Sosi huyo aliendelea kudai kuwa nyumbani kwa akina Jokate ambaye aliapa kuwa lazima mwaka huu aolewe, kulikuwa na wageni wengi ambao miongoni mwao ndiyo waliopeleka posa.

“Mh! Watu ni wambeya jamani! Mimi nilienda kwetu na ninatarajia kufanya kitu kikubwa huko Songea mtakisikia ‘soon’,” alisema Jokate huku akicheka.