WAIGIZAJI ‘the big names’ wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na
Jacob Steven ‘JB’ wamezua minong’ono baada ya kugandana kimahaba hadi
wakawakera maustadhi.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri katika Kijiji
Cha Kwadelo wilayani Kondoa, Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo
mastaa hao walikwenda kuzindua mpango wa Kilimo Kwanza, Ajira kwa Vijana
ulioongozwa na Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omary Kariati.
Waigizaji
hao walionekana kupeana ‘kampani’ kwa kila walichokifanya, huku kila
mmoja akigandisha mkono kiunoni kwa mwenzake na kushikanashikana
hadharani huku Wema akideka na ‘kale kasauti kake kanakoweza kumtoa
nyoka haraka pangoni’.
“Hawa wasanii wetu bwana, hebu waone wale (Wema na JB), muda wote
wameshikana vile. Mh! Ndiyo nini sasa?” alisikika mmoja wa maustadhi
aliyejitokeza katika uzinduzi huo.
Wakiwa mashambani, ulifika wakati
wa mastaa hao kulima kwa kutumia trekta ambapo JB alionekana akimbeba
Wema na kumsaidia kupanda kwenye trekta kisha akamsaidia tena kushuka
baada ya kumaliza kazi.
WEMA, JB WAWAKERA MAUSTADHI

