Katika hali isiyo ya kawaida, kichanga cha siku sita cha jinsi ya kike
kimekutwa kimetelekezwa na mtu asiyefahamika juu ya mti ambapo
kiliokotwa na mpita njia katika kijiji cha Losimingori kwa Laoshiye,
wilayani Arumeru, ambapo kilikuwa kumeviringishwa kwenye mfuko wa
plastiki.
Alisema baada ya tukio hilo, msamaria huyo alitoa taarifa kwa uongozi wa eneo hilo mbapo yeye na viongozi wengine walifika na kushuhudia kichanga hicho ambapo kilionekana chenye afya njema.
Aidha, mtendaji huyo alisema kuwa haikufahamika mara moja mtu aliyehusika na unyama huo wa kikitelekeza kichanga hicho ambapo pamoja na mambo mengine uongozi uliamua kumkabidhi mwanamke huyo kwa lengo la kukihudumia huku taratibu zaidi za kumsaka mama yake zikiendelea.
“Uongozi wa kijiji unaandaa utaratibu wa kukipeleka hospitali ili kuchunguza afya yake. Tukio hilo limewashtua wakazi wa eneo hili ambao ni jamii ya wafugaji,” alisema mtendaji huyo na kuongeza kuwa wanafanya msako katika eneo hilo na jirani kuweza kumbaini mwanamke yeyote aliyekuwa na ujauzito hivi karibuni na atakayebainika kufanya unyama huo atachukuliwa hatua za kisheria.