Msanii wa filamu na muziki Bongo Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ anasema
kuwa muziki anaofanya na kundi lake la Scopion Girls ni wa muda tu kama
anafanya mazoezi, anafanya hivyo kwa sababu mara nyingi makundi ya
muziki wa kizazi kipya hayadumu kwa mantiki hiyo iwapo kundi lao
litakufa ataingia rasmi katika kuimba muziki wa Injili.
“Nafanya
muziki nikiwa na kundi lengo ni kudumu kwa muda mrefu lakini kama
itatokea kuvunjika kundi langu la Scopion Girls basi nitaimba nikiwa
pekee yangu lakini si muziki huu wa kidunia bali nitamwimbia Mungu wangu
kwa kuimba muziki wa Injili kwa sababu natamani sanakuokoka,”anasema Jini Kabula.
jini kabula akipigana denda na jack.
Jini
Kabula ambaye ni mzazi mwenzake na mwigizaji na mkurugenzi wa Tuesday
Entertainment Ltd Mr. Chuzi pamoja na kuimba muziki pia ni mwigizaji
nyota aliyejichukulia umaarufu katika tamthilia ya Jumba la Dhahabu na
kushiriki katika filamu nyingi zinazoandaliwa na kampuni mbalimbali.
"NATAMANI KUOKOKA NA KUANZA KUIMBA NYIMBO ZA INJILI"...JINI KABULA

