skip to main |
skip to sidebar

11:50 PM

Anonymous
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), (kushoto)
akisalimiana na Mhe. Andry Rajoelina, Rais wa Madagascar mara baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini
Dar es Salaam tarehe 11 Januari, 2013. Mhe. Rais Rajoelina yupo nchini
kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano unaoendelea wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na
Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC-TROIKA).
Mhe. Rais Rajoelina akiwa amefuatana na Mhe. Membe mara baada ya kupokelewa.
Mhe. Rais Rajoelina akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili.
Mhe. Rais Rajoelina akipita katikati ya Gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake huku akisindikizwa na Mhe. Membe.
Mhe. Rais Rajoelina akiwa na Mhe.
Membe wakifurahia burudani ya ngoma za utamaduni zilizokuwepo Uwanjani
hapo mara baada ya kuwasili.