Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodegar Tenga amesema
hawezi kugombea tena nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo
unaotarajia kufanyika February 24 mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Tenga
amesema wakati anaingia madarakani miaka minne iliyopita alikuwa na kazi
ya kufanya, ambayo ilikuwa ni kujenga taasisi ya soka nchini, na kwamba
hawezi kuendelea tena kwani uongozi ni kijiti na kwamba huu sasa wakati
wa kukimbizwa na mtu mwingine.
“Nimekaa madarakani kwa miaka minane kwakweli ni miaka mingi
sana,tangu mwaka 2004 ambapo wakati huu kulikuwa na ajenda maalum ya
kuleta mabadiliko ya msingi katika soka”alisema Tenga.
TENGA ASHINDWA "URAIS" WA TFF

