MWIGIZAJI, mtunzi na prodyuza wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ‘Stara’
amesema kuwa wakati mumewe, marehemu Juma
Kilowoko ‘Sajuki’ akiumwa
kabla ya kukutwa na umauti, ilibaki kiduchu ageuke kichaa.
Prodyuza huyo mkubwa wa filamu za Kibongo alisema kuwa ilifika ‘taimu’
akawa anapiga kelele ovyo ndani ya nyumba yao kutokana na kubanwa na
mawazo.
Alifunguka kuwa kila mumewe alipomuona na hali hiyo alikuwa akimuomba atulie na kumwambia akiendelea atakuwa chizi.
“Sajuki alikuwa akiniambia ananionea huruma sana kutokana na hali niliyokuwa nayo.
“Yaani
nilijua naaga dunia kiukweli kwani nilikuwa nawatumia watu meseji
kuwaomba msamaha kama nimewakosea kwa sababu kila nilichofanya kilikuwa
hakiendi,” alisema Wastara.
Wastara alisema kuwa aliichukia wodi
aliyolazwa mumewe katika Hospitali ya Muhimbili, Dar kwani ndani ya
wodi hiyohiyo aliwahi kulazwa mama yake mzazi ambaye naye alifia wodini
hapo miaka ya nyuma.
WASTARA: UGONJWA WA SAJUKI, NUSU NIWE KICHAA

