MAMBO
Vipi mdau wangu, kama kawaida tunazidi kusonga mbele kwa kuwaletea
mastaa ambao tayari Mungu amewajalia watoto. Kutokana na maombi ya
wasomaji wengi wiki iliyopita kumtaka mtangazaji mahiri wa Kipindi cha
Mitikisiko ya Pwani katika Redio ya Times Fm, Hadija Shaibu ‘Dida’, leo
nimewaletea.
Hadi sasa Dida ana mtoto wa miaka nane aliyempatia jina
zuri la Samira, mwenyewe anasema kuwa kwa mwanaye, mtu humuelezi kitu
chochote. Twende katika mahojiano niliyofanya naye hapa chini:
SAUALA LA VIBOKO
“Unajua kama watoto jinsi walivyo siku zote ni
watundu lakini suluhisho siyo adhabu ya kuwapiga, mimi mara nyingi
napenda sana kuzungumza na mwanangu pindi anapokosea na ni rahisi
kunielewa maana mimi mwenyewe nikisikia hata mtoto wa jirani anapigwa,
huwa naumia sana.”
ANAPENDA KUSAFIRI NAYE
“Katika safari zote ninazosafiri hasa za
nje ya nchi, huwa sijisikii raha sana kama nikimuacha mwanangu. Mara
nyingi nikiwa na muda mzuri huwa napenda kusafiri naye maana huko
tunaweza kuongea naye mambo mbalimbali ya kumfunza kwa maana tunakuwa
sehemu yenye utulivu.”
MTOTO WAKE HAPENDI KUMUONA AMECHUKIA
“Kitu ambacho mwanangu
hapendi kukiona kutoka kwangu ni mimi nikiwa nimekasirika, atajitahidi
kwa hali na mali kunifanya nicheke au hata ajue ni sababu gani
imenifanya
nikasirike.”
MWANAYE FULL VITUKO
“Kitu ambacho mtoto wangu ananipa raha ni pale
anapokutana na mtu ambaye hamfahamu, kitu cha kwanza atamuuliza,
unamjua Dida wa Mchomeeeee? Hahahaha!”
HAPENDI MWANAE AWE MTANGAZAJI
“Kwa kweli kuna msemo usemao maji
hufuata mkondo lakini mimi sipendi mwanangu awe mtangazaji hususan
taarab kwa sababu kuna mabifu mengi sana bora hata atangaze vipindi
vingine aniache mimi mama yake nikomae nao.”
source:GP
DIDA: SIJAWAHI KUMTANDIKA VIBOKO MWANANGU

