
Omotola
IMEKUWA ni jambo la kawaida kabisa kuona ndoa za mastaa zikivunjika.
Kashfa za ufuska pamoja na nyingine kadha wa kadha zimekuwa zikitajwa
kama sababu za kusambaratika kwa ndoa hizo.
Pamoja na
kuwako kwa idadi kubwa ya ndoa za mastaa zinazovunjika, wapo wengine
ambao ndoa zao zimekuwa mfano mzuri, unapenda kuwafahamu?
Ndoa ya mwigizaji Joke Silva ni miongoni mwa ndoa chache za Nollywood zilizoweza kukaa kwenye mstari bila ya mgogoro.
Tofauti
na ndoa nyingine za Nollywood, ya kwake imeishi kwa kipindi kirefu bila
kuwa na kashfa. Mume wa mwigizaji huyu, Olu Jacobs, ni nguli wa maigizo.
Ndoa yao
inatajwa kuwa iliyojawa na furaha na baraka tele. Ndoa hiyo kwa sasa ina
miongo mitatu na sasa Joke anaonekana kama kioo kwa wanawake wengi
Nigeria hususan vijana.Kuisoma zaidi