Tunaendelea
kuzihesabu siku kadhaa kuikamilisha mbio ya kuumaliza mwaka 2013 Mungu
akipenda huku mengi yakiwa yamekamilika na mengine yakiwa pending.
Binti
Komando, Anaconda, Lady Jay Dee bado hajakamilisha mpango wa kuuweka
wazi wosia wake, lakini hivi karibuni watanzania na wadau wa muziki
wanaweza kuushuhudia wosia huo kabla hatujauanza mwaka 2014.
Hii inatokana na tweet ya Jide ya December 18,2013.
Katika
hatua nyingine, Yahaya hit maker ameweka wazi moja kati ya ndoto ambazo
anatamani sana kuzitimiza ikiwa ni pamoja na kukutana na daktari wa
midundo duniani ‘Dr. Dre’, na mkali wa R&B Usher Raymond.
Jide ameandika kwenye blog yake:
“Kati
ya NDOTO zangu mbili kubwa zilizobakia hapa duniani ni kukutana na watu
hawa wawili Dr. Dre na Usher Raymond 2013 hiyoooo inayoyoma ndoto
imekuwa ndoto, hebu tusaidiane kusali
WAFAHAMU WASANII WAKUBWA KUTOKA NCHINI MAREKANI AMBAO LADY JAY DEE ANA-DREAM KUFANYA NAO KAZI

