
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Snura Mushi ‘Mama Majanga’ ametoa ya moyoni na kumshukuru aliyekuwa rafiki yake wa damu, Wema Sepetu kwa kuwa ndiye aliyembunia vazi la muziki na fedha ya kurekodi wimbo wake wa kwanza.

“Namshukuru Wema, kwani alihusika sana kwenye wimbo wangu wa kwanza wa ‘Shogaake Mama’ kwani fedha yake ndiyo ilitumika kurekodi wimbo huo pia aliingiza sauti yake kwenye wimbo huo, alinibunia vazi la shoo yangu ya kwanza ambalo ninaliendeleza mpaka sasa,” alisema Snura.