LULU.
Kesi
ya mauaji ya kutokukusudia inayomkabili msanii wa filamu nchini,
Elizabeth Michael `Lulu’, imepokelewa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar
es Salaam na kusajiliwa kwa namba 125 ya mwaka 2012.
Kwa mujibu
wa habari zilizopatikana mahakamani hapo, kesi hiyo imepokelewa kutoka
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na inasubiri kupangiwa Jaji na tarehe ya
kuanza kusikilizwa.
Awali Lulu alikuwa akikabiliwa na mashitaka
ya kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba, kwa kukusudia lakini baada ya
upande wa mashitaka kukamilisha upelelezi alibadilishiwa mashitaka na
kuwa kuua bila kukusudia.
Kesi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Augustina Mmbando, katika hatua
za awali na Lulu hakuruhusiwa kujibu mashitaka yanayomkabili kwa kuwa
Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Kwa mujibu wa sheria, kutokana na Lulu kushitakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia, anaweza kupata dhamana.
KESI YA LULU MICHAEL SASA RASMI MAHAKAMA KUU

