SHILOLE AMKUFURU MUNGU..


 

Msanii wa filamu na muziki Bongo , Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amewaacha watu midomo wazi baada ya kufanya kisomo na watoto yatima mchana na usiku akaangusha pati iliyokuwa na matukio ya kumkufuru Mungu.
Matukio hayo yalijiri Desemba 18, mwaka huu ambapo Shilole alikuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa bila kutaja umri.

 

Majira ya mchana , dada huyo alifanya kisomo nyumbani kwake Kinondoni, Dar pamoja na watoto yatima wa Kituo cha Magomeni kisha akapata nao msosi na kuwapa msaada wa vyakula.

Wakati wa mchana, Shilole alionekana akiwa ndani ya mavazi nadhifu yaliyomsitiri vilivyo , akila pamoja na watoto hao na wageni wengine waalikwa wakiwemo wasanii wenzake.
Usiku  wake baada ya matukio ya mchana, sherehe ilihamia katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambapo kulikuwa na matukio kibao ya kumkufuru Mungu.




 


Twitter Delicious Facebook Digg Favorites More